Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, June 3, 2014

Kuelekea Kombe la Dunia 2014: Riccardo Montolivo kulikosa Kombe la Dunia baada ya kuvunjika mguu

Kiungo wa Italia Riccardo Montolivo atalikosa Kombe la Dunia baada ya kuvunjika mguu wakati wa mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliomalizika kwa sare ya 0-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika dimba la Craven Cottage.
Mchezaji huyo wa AC Milan, 29, aliondolewa uwanjani na machela baada ya kukumbana na mlinzi wa Reading Alex Pearce.
Daktari wa timu ya Italia Enrico Castellacci amesema: "Sijaona picha ya X-ray ili kuelezea jambo hili, lakini kwa mfupa uliovunjika unaweza kutegemea upasuaji."
Italia watakutana na England, Uruguay na Costa Rica kwenye Kundi D.
Montolivo, aliichezea Italia mchezo wa 58 kwa dakika nane kwenye mchezo wa kirafiki kujiandaa na fainali za Kombe la Dunia, lakini aliondolewa uwanjani akiwa juu ya machela na kuwahishwa katika hospitali moja mjini London kwa ajili ya X-rays, ambayo ilithibitisha uharibifu huo kwenye mguu wake.
Nafasi yake ilichukuliwa na kiungo wa zamani wa Liverpool Alberto Aquilani, ambaye hakurudi tena dimbani baada ya mapumziko akidai kutojisikia sawa.
Mchezaji mwenza wa Aquilani katika klabu ya Fiorentina Giuseppe Rossi anaweza kujihakikishia nafasi katika kikosi cha Italia kitakachokuwa na wachezaji 23 kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil, licha ya kucheza kwa dakika 70 akirejea kutokana na maumivu ya goti.
Worried: Italy captain Riccardo Montolivo was injured in the friendly against Ireland

Painful: Montolivo came off worse in a challenge with Ireland defender Alex Pearce in the first-half

Injury: Montolivo received treatment on the pitch before eventually leaving on a stretcher


Something to prove: Italy coach Cesare Prandelli named a changed side for the game against Ireland

Star man: Mario Balotelli was named on the bench for Italy's game against Ireland

No comments:

Post a Comment