WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya CECAFA
Nile Basin Cup, Mbeya City fc wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0
dhidi ya Victoria University ya Uganda katika mchezo wa robo fainali
uliomalizika dakika chache zilizopita mjini Khartoum.
Mbeya City wametolewa katika michuano hiyo wakiwa
wameshinda mechi moja, kufungwa moja na kutoka suluhu mechi moja katika hatua
ya makundi.
Lakini wamepoteza mechi ya pili katika mashindano
haya baada ya kufungwa hatua ya robo fainali na kufungashiwa virago.
Afisa habari wa Mbeya City fc, Freddy Jackson
amesema wanashukuru kwa kilichotokea kwani ndio matokeo ya mpira wa miguu.
Freddy amesema wachezaji wamejitahidi kucheza kwa
juhudi, lakini hawakuwa na bahati.
“Ndugu tunashukuru kwa maombi yenu, alichotupangia mungu ndicho tulichopata. Mechi imemalizika , Mbeya city O victoria 1, hivyo
basi tumeyaaga mashindano”. Amesema Freddy.
No comments:
Post a Comment