Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 4, 2014

NYOTA WA COLOMBIA FALCAO KUZIKOSA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA



Falcao akiwa na kocha wake Jose Pekerman kwenye mmkutano na waandishi wa habari

MASHABIKI wa Colombia wamepagawa na taarifa kwamba nyota wao Radamel Falcao atazikosa fainali za kombe la dunia za mwaka huu nchini Brazil.

 Kocha wa timu ya Colombia, Jose Pekerman jana jumatatu alitangaza kikosi chake katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Buenos Aires, nchini Argentina.

 

Falcao alipata majeruhi kubwa ya goti akiwa katika majukumu ya kuitumikia klabu yake ya Monaco mwezi januari, na ameachwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambapo kocha wake amesema hatakuwa tayari.
Nyota huyo wa zamani wa Atletico Madrid  alisajiliwa kwa dau kubwa mno majira ya kiangazi mwaka jana, lakini kutokana na majeruhi aliyopata alikosa matumaini ya kulitumia taifa lake katika fainali za kombe la dunia mwaka huu. Pekerman alisema wiki iliyopita kuwa atasubiri mpaka siku ya mwisho na dakika ya mwisho  ili kufanya maamuzi juu ya Falcao baada ya kuona anaimarika kidogo kidogo, huku akionana na madaktari wake, na mwisho wa siku, hapo jana alifanya maamuzi kinyume na maneno yake.


No comments:

Post a Comment