Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kuvuka
hatua ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa
huru ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani.Stars leo ilikuwa inacheza
Zimbwabwe kwenye mchezo wa marudiano baada ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja
wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada
ya kulazimisha sare ya 2-2.
Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars
kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub 'Cannavaro' dakika ya 28.Muda
mchache baadae Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili dakika ya 46,
kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.Mpaka
refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa Tanzania
wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji.
No comments:
Post a Comment