17 Juni 2014.
1 :0 UTANGULIZI
Ndugu
wana habari na ndugu Watanzania, kwa kutambua mchango wangu mkubwa
ambao nimkuwa nikiufanya katika ujenzi wa vyama vya siasa hasa Upinzani
hapa nchini, ni dhahiri nimekuwa mjenzi wa vyama kuliko mafanikio ya
wananchi. Nimegundua mengi sana na kujifunza mengi sana juu ya hivyo
vyama vyetu vya Siasa, tunapotafuta demokrasia katika nchi yetu sio tu
kuwa huru kwa kila jambo bali kuwa na UTU kwa watu tunaowatafutia
Demokrasia ya kweli, hatuwezi kusema nchi hainademokrasia kama
hatujatenda haki kwa wanachama au wananchi wetu.
SABABU ZA KUJIUDHURU UANACHAMA NA NYADIFA ZOTE ZA UONGOZI.
2
:0 AJALI YA GARI Mwaka jana June 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa
Udiwani Wilayanisengerema Kata ya Nyampulukano na mimi nikiwa msimamizi
wa Uchaguzi huo mdogo wa marudio, jumamosi ya kuamkia uchaguzi tulipata
ajali ya gari tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura na mimi nilikuwa
kiti cha mbele cha gari na nikapata maumivu makali sana, japo nilipewa
huduma ya kwanza lakini baada ya hapo sikupata matibabu stahiki kitu
ambacho mpaka sasa, nisingeweza kulaumu kama hawajui lakini wanajua fika
viongozi wenzangu, na ukizingatia wakati ule nilikuwa Katibu wa
Mahusiano na Uenezi Taifa kitengo cha Vijana.
Kutokana
na hali kuwa si nzuri na kufikia kuona nalalamika ujue kabisa hali si
nzuri ki afya, jambo la msingi kwa wenzangu hata kama wanahisi na makosa
lakini jambo la Busara ni UTU kwanza wakumponya aliye mgonjwa ndipo
busara zingine zinafanyika, kiukweli nasikitika sana na ninaumia sana
kwa tukio hili maana ile ilikuwa ni kazi ya chama na siya mtu, ina maana
hata Elfu kumi tu nayo ni ngumu ? kweli hapa tujiulize sasa, na ndio
maana naumia sana kwa hilo, kwa hili mimi naona kama wamenitelekeza na
kuniachia familia yangu mzigo.
Nashauri
tu kuwa vijana wenzangu wa Kitanzania tunapo jiunga na vyama vya Siasa
tuchunguze UTU kwanza kabla hatujafikia maamuzi na tusiwe washabiki
wasiasa bila kujua hatima yetu kimaisha, nashauri kama vijana tuwe
tunasapotiana kwenye matatizo maana leo limemkuta Kisandu kesho linakuja
kwako. Nimejaribu hatakuomba msaada kwa baadhi ya viongozi rafiki
msaada wa aina yoyote bila mafanikio.
USHAURI
WANGU kwa chama changu NCCR – Mageuzi naomba kama hili limetokea kwangu
basi lisijirudie kwa mwingine kwani hata Mungu hapendi kuona hali kama
hizo.
Kutokana
na hili la matibabu ndugu na familia yangu wamenishauri niachane na
Siasa za vyama ili waweze kuona wananisaidia vipi, kimsingi naungana na
ndugu zangu na kukubali ombi lao kuliko kuumia namna hii. Naomba
msamaha kwa viongozi wenzangu pale tulipo kwazana na mimi na wasamehe
pale walipo nikosea japo nabaki na maumivu ya kiafya.
3 :0 KATIBA MPYA
Kwa
upande wa swala la KATIBA MPYA, huu mchakato si wa mtu mmoja au watu
kadhaa bali ni mchakato wa Watanzania wote. Swala la Muundo wa Muungano
si swala la CCM wala UKAWA bali ni letu sote, hapa ningeshauri tu
kuepuka mvutano baina ya serikali mbili au Serikali tatu, wakakaa pamoja
na kufikia maridhiano yenye Busara ili tupate Katiba mpya inayoendana
na mazingira ya Kitanzania. Pia lazima wawakilishi wetu Bunge la
Katiba watambue kuwa maoni ya Serikai mbili ni ya Wananchi na Maoni ya
Serikali tatu nayo pia ni ya Wananchi hivyo Busara ndio itumike
kurejesha Umoja wetu wenye katiba ya pamoja.
4 :0 KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA HUU
Viongozi
wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo badala ya
kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha maana kama
tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote bali serikali
ikosolewe kwa kupewa solution.
5:0 UKAWA
Hakuna
dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi, Baba au Mama akibagua baadhi ya
watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi inayohitaji kukemewa.
Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si wazalendo kabisa
wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama. Vyama vya Siasa vipo 23,
vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo wote ni wapinzani eti
UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria kama ni uchaguzi Mkuu,
vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana hata robo haijafika.
Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki kabisa na si vitendo bali
ni Umoja ndani ya Mtengano. Wakiweza
kuungana
vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na siasa na
hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya vyama
itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama vitatu
na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote 22 vya
Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu.
6:0 FIKRA MBADALA
Vijana
wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya kisiasa
na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na Uzalendo bila
kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua vyama bali tuchague
viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama.
7:0 MAPUMZIKO
Kwa
sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya
kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba
nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale
nitakapooona inafaa na sijui ni lini.
Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na Mungu atupe uzima wa maisha marefu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.
MWL. DEOGRATIUS KISANDU
ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA NCCR – MAGEUZI
17 / 06 / 2014
0786 025 609
No comments:
Post a Comment