Wasanii hao ni ndugu waliozaliwa Mapacha na huwa wanafanya Muziki wao kwa pamoja ndani yake kuna "K-Wa Mapacha" na "D-Wa Mapacha"
Mapacha walipata exclusive interview ndani ya kipichi cha XXL na watangazaji wa kipindi hicho (B-12, Adam Mchomvu na Dj Fetty) walipo jaribu kuwauliza kwanini walitunga Mixtape mbili kuwa diss watangazaji wa clouds fm na kwanini walikua wanawapa vitisho vya kuwadhuru mtaani? Mapacha walikiri kuwa mwanzo walikosea na lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho ndio sababu wakaamua kuomba suluhu ili kuyajenga kama zamani ambapo nyimbo zao zilikua zinachezwa sana na kuwafanya kuwa moja kati ya Mastar wanaoingiza mkwanja mrefu kutokana na muziki kama wasanii wengine wa sasa, Mapacha wakaongeza kuwa hawaoni aibu kwa uamuzi huu wa sasa kama watu wanavyofikiria na kama kuna vinega wengine wanawachukia kwa uamuzi huu basi wao binafsi hawajali wanachoangalia ni maendeleo ya maisha yao.
Moja kati ya vitu ambavyo walipitia kipindi cha miaka mitano ya Beef yao na Clouds fm ni pamoja na kutengwa na jamii kutokana na taswira yao kuonekana kuwa si wastaarabu ni watu wa matusi kiasi cha kwamba hata wasanii wenzao waliwaogopa hata makampuni kuhofia kuwapa kazi za matamasha walikua hawaaminiki.
Licha Vinega enzi zao kurusha makombora mazito kwa Clouds fm, kituo cha Radio cha Clouds fm hakikuwahi kuwajibu hata mara moja.
Mapacha si watu wa kwanza kutoka kundi la vinega kupatana na Clouds, alianza Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Mr 11 a.k.a Sugu mwaka 2012 aliamua kuzika beef yake kwa kupatana Mkurugenzi wa uzalishaji wa Clouds Fm Ruge Mutahaba.
Throw Back february 2012 |
No comments:
Post a Comment