Vijana 65 wa Tanzania wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini
China baada ya kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za
kulevya.
Vijana hao ni kati ya zaidi ya 403 wa Tanzania
wanaoshikiliwa katika nchi mbalimbali duniani kwa tuhuma ya kujihusisha na
biashara hizo.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, mjini Dodoma wakati akizungumzia
Maadhimisho ya Siku Dawa za Kulevya Duniani yanayofanyika Juni 26 kila mwaka.
Lukuvi alisema kuwa kwa mwaka huu maadhimisho hayo ya kesho,
kitaifa yatafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nzovwe jijini Mbeya na
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
“Tangu mwaka 2008
kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wenye asili ya Kitanzania kujihusisha na
biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi, mpaka hivi sasa idadi
yao ni kubwa kiasi cha kufikia zaidi ya 400, na wanashikiliwa katika nchi
mbalimbali ambazo pia adhabu zao zinatofautiana kulingana na sheria za nchi
hizo”
alisema Lukuvi.
No comments:
Post a Comment