Pichani ni Jengo litakalojengwa jijini Dar es salaam na litagharimu Dola za kimarekani milioni 77,kutakuwa na hoteli ya hadhi ya Nyota Tano, Ofisi za Biashara, kutakuwa na Sehemu ya kuegesha magari, jengo hili litatakuwa kivutio kwa Wawekezaji na Utalii.
Baadhi Malori na Vifaa vingine vya kutendea kazi vikiwa tayari kuahiria ujenzi huu unaanza mara moja baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi kukamilika.
Mama Maria Nyerere akiwasili kwenye sherehe ya uwekaji jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo la Malimu Nyerere Foundation Square
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamini Mkapa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Cleopa Msuya wakati wa shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa jengo refu la ghorofa la Mwalimu Nyerere Foundation.
Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuwekwa jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam.
Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (kulia) wakijippongeza baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakimwaga mchanga kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam,Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akibadilishana mawazo na Profesa Shivji pamoja na Wazee wengine wakati wa shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi wa Ujenzi wa jengo la Mwalimu Nyerere Foundation Square.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku akihutubia wakati wa Uwekaji wa jiwe la msingi wa jengo la Mwalimu Nyerere Foundation Square.
Picha ya Pamoja baada ya zoezi la uwekaji wa jiwe la Msingi kukamilika.(Picha na Adam Mzee)
No comments:
Post a Comment