Aliyekuwa mmiliki wa timu ya mpira wa vikapu LA Clippers,
ambaye amezongwa na balaa za kisheria, Donald Sterling, amekubali kuiuza klabu
hiyo.Bwana Sterling ameiuza klabu hiyo kwa aliyekuwa mkuu wa kampuni ya
Microsoft Steve Ballmer, kwa dola bilioni 2.
Bwana Sterling amekuwa akikabiliwa na shutuma za ubaguzi wa
rangi.Ametangaza pia kuwa ataondoa kesi aliyowakilisha dhidi ya shirikisho la
mpira wa vikapu nchini Marekani NBA, ya kudai ridhaa ya dola bilioni moja
akisema kuwa shirikisho hilo limekiuka haki zake za kikatiba.Shirikisho hilo la
NBA limemuwekea marufuku ya maisha bwana Sterling kutohudhuria mechi zozote za
mchezo huo, kufuatia kanda zilizotolewa akimtusi aliyekuwa mpenzi wake kwa
matamshi ya kibaguzi wa rangi.Pia bwana Sterlig amepewa hakikisho kuwa NBA
haitamfungulia mashtaka yoyote. Sasa kinachosubiriwa ni asili mia 75 kati ya
wamiliki washirikishi 29 waliosalia wa klabu hiyo kuidhinisha uuzaji huo.CHANZO BBC




No comments:
Post a Comment