Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, June 7, 2014

TAZAMA PICHA ZA TIMU YA TAIFA YA UHOLANZI WAKIKWEA PIPA KWENDA BRAZILI



Wanaondoka: Wesley Sneijder (kushoto) akipozi kwenye picha na mke wake Yolanthe wakati kikosi cha Uholanzi kikijiandaa kwenda Brazil.

WACHEZAJI wa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kinachokwenda kushiriki kombe la dunia 2014 nchini Brazil mwaka huu walionekana wenye tabasamu kubwa wakati wakijiandaa kupaa angani na ndege licha ya kuagana na wapenzi wao jana alhamisi.

Nyota hao wa Uholanzi walipozi katika picha na wake na watoto zao kwenye hoteli ya timu hiyo kabla ya kwenda uwanja wa ndege wa  Schipol airport tayari kwa kuanza safari ya kwenda Brazil.

Wesley Sneijder na Dirk Kuyt walionekana kuwa karibu zaidi na familia zao huku wakifurahi kwa dakika za mwisho mwisho.



Dirk Kuyt (kushoto) akimuaga mke na mtoto wake.



Mlinda mlango wa Swansea,  Michel Vorm  aliungana na kikosi cha Uholanzi kwenda Brazil



Mtu muhimu: Mashabiki wa Uholanzi wanamtegemea zaidi Robin van Persie (katikati)



Kila la kheri: Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal akiwapungia mkono mashabiki kabla ya kukwea pipa kuelekea Brazil.



Jamani tunasepa!: Arjen Robben (katikati) akiwasili uwanja wa ndege wa Schiphol airport uliopo karibu na Amsterdam.

No comments:

Post a Comment