Fred alikuwa mbuzi wa kafara kwa mashabiki katika hatua ya mwisho ya mashindano.
Fred amestaafu soKa la kimataifa baada ya Brazil kuharibu mno katika fainali za kombe la dunia ndani ya ardhi yake mwaka huu.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30 ambaye ameichezea nchi yake mechi 39, amekuwa mbuzi wa kafara kwa mashabiki wa Brazil waliomkosoa kuonesha kiwango cha chini.
Brazil ilifungwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali jumanne ya wiki iliyopita na juzi jumamosi walifungwa mabao 3-0 na Uholanzi katika mchezo wa mshindi wa tatu.
Fred alikuwa mfungaji bora wa mashindano ya kombe la bara mwaka jana ambapo Brazil iliibuka mabingwa.
Fred kila alipogusa mpira katika kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani, Belo Horinzote alikumbana na kelele za kuzomewa.
Hatua hii ya kustaafu imekuja baada ya mwaka mmoja tu kupita tangu mshambuliajia huyu wa Fluminense ashinde kiatu cha mfungaji bora wa kombe la mabara akiwa na mabao matano.
Fred alifunga bao lake la kwanza katika mechi ya kirafiki ya Brazil dhidi ya UAE ambapo wazee wa samba walishinda mabao 8-0 mwaka 2005, na alifunga mabao mawili katika fainali za kombe la dunia mwaka huu.
Rekodi nzuri: Fred ameichezea Brazil mechi 39 na kufunga mabao 18 tangu 2005.
No comments:
Post a Comment