Bhangi ni halali katika majimbo 23 ya Marekani
Matumizi ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa
katika jimbo la Washington nchini Marekani.Washington ni jimbo la pili nchini
Marekani kuhalalisha Bangi , baada ya Colorado, ambako jimbo hilo linajipatia
mamilioni ya dola kila mwezi kwa kutoza ushuru biashara za Bangi kwa
wanaoitumia kujiburudisha.
Hata hivyo utaratibu wa kuuza bidhaa hiyo utadhibitiwa
ipasavyo katika jimbo hilo.
Ni maduka 25 pekee yaliyoruhusiwa kuuza Bangi hadi sasa,
ingawa maafisa wanaamini kuwa idadi ya maduka huenda ikaongezaka na kufika
miamoja.
Katika sehemu zingine za Marekani, majimbo 23 yanaruhusu
matumizi ya Bangi kwa sababu za kimatibabu.


No comments:
Post a Comment