Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, July 14, 2014

MFANYABIASHARA MAARUFU AUAWA MOMBASA




Watu wawili wenye bunduki wamemuua mfanyabiashara maarufu mjini Mombasa anayeshtakiwa kwa ugaidi nchini Kenya.

Mohamed Shahid Butt alikuwa ndani ya gari lake akitokea kwenye uwanja wa ndege siku ya Ijumaa, ambapo gari lake lilizuiwa na gari jingine kabla ya watu wawili kumpiga risasi.
Bwana Butt alikuwa afike mahakamani mwezi ujao kujibu mashtaka ya tuhuma za kufadhili itikadi kali kwa vijana wa Kiislam. 
Kumekuwa na mfululizo wa mauaji ya watu wanaodaiwa kujihusisha na Uislam wenye itikadi kali katika eneo la pwani karibu na Mombasa. 
Wanaharakati wa haki za binaadam wameituhumu serikali ya Kenya kwa kuhusika na mauaji hayo, kwa kuwa kesi chache zimeweza kushughulikiwa.

Mkuu wa polisi wa kaunti ya Mombasa, Richard Kitur, ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa bwana Butt alikuwa ametoka kumpokea mwanaye wa kiume kutoka uwanja wa ndege, kabla hajapigwa risasi. 
Bwana Butt alifikishwa mahakamani mwaka jana akituhumiwa na mamlaka kwa uchochezi na kufadhili shughuli za kigaidi.
Katika miaka miwili iliyopita, Waislam watatu wanaofahamika sana, na ambao walikuwa wakijulikana kujihusisha na itikadi kali wameuawa. 
(Picha- KTN)

No comments:

Post a Comment