Mwanamume mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye
hospitali ya taifa ya Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na
mzigo wa dawa za kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake.Huyu jamaa alikua
anazisafirisha hizi dawa kutoka Lagos kwenda Bangkok lakini ghafla akaanza
kupata maumivu baada ya kuchelewa kufikisha mzigo aloubeba tumboni mwake baada
ya ndege waliyokua wakisafiria kutua Nairobi kwa dharura.Ilitua kwa dharura
baada ya rubani kuumwa ghafla hivyo kulazimu ndege kutua Nairobi kisha abiria wote
kupelekwa hotelini na hapo ndio Mnigeria huyu akaanza kuhisi maumivu makali
tumboni.
Simon Ithae ambae ni mkuu wa mawasiliano hospitali ya
Kenyatta amesema ‘alitueleza amemeza vidonge na alikua akiamini ndicho chanzo
cha maumivu hivyo alipoona hawezi kustahamili aliita Polisi akidai
ameumizwa na
anahitaji kupelekwa hospitali lakini lengo lake ni apange njama na madaktari
kutoa dawa za kulevya bila yeye kukamatwa na aendelee nazo na safari lakini
mipango yake haikufanikiwa kwa sababu Madaktari walimpa chakula ili kutoa dawa
hizo na kisha wakawapa taarifa Polisi.
No comments:
Post a Comment