Sasa imethibitika kwamba mtoto huyu rubani aliekua anataka
kuweka rekodi ya dunia kwa kuwa rubani mdogo aliesafiri umbali mrefu, amefariki
dunia na mwili wake kupatikana baada ya ajali ya ndege hiyo iliyotokea baharini
Jumanne usiku ambapo Baba yake ambae walikua pamoja hajulikani alipo
Marehemu Haris katikati wakati akizungumzia maandalizi ya
safari hiyo.
Mpaka sasa chanzo cha kuanguka kwa ndege hii hakijajulikana
ambapo Hiba Suleman ambae ni dada wa marehemu amesema ‘tunatumai baba yetu yu
hai, tutaendelea kusali mpaka tutakapopata jibu la mwisho… ‘
Wawili hawa walikua na blog yao ambayo walikua wanapost vitu
mbalimbali zikiwemo picha za wanakopita au kutembelea ambapo post yao ya mwisho
kuiweka ilikua ni July 20 2014 Bali Indonesia.
Watu mbalimbali waliokua wanawafatilia wameanza kutoa salamu zao za rambirambi kwa familia baada ya kupokea taarifa za ajali waliyoipata ambapo mmoja wa waliokua wanawafatilia ni Private Pilot Ahmed.Ahmed amesikitishwa na ajali waliyoipata na kusema imeuma zaidi hasa kwa sababu ndio ilikua karibu wamalize safari hii ambayo ni rekodi ya dunia.CHANZO MillardAyo
No comments:
Post a Comment