Shambulizi Gaza laua watu 15 katika soko
Takriban watu 15 wameuwa na wengine 160 kujeruhiwa vibaya
katika shambulizi kali la angani lililotekelezwa na Israeli kwenye soko moja
huko Gaza .
Kwa mjibu wa viongozi wa Kipalestina mlipuko mkubwa ulilipua
soko moja la Shejaiya la kuuza matunda na mboga ambalo kwa kawaida huwa na
idadi kubwa ya watu, mashariki mwa Gaza.
Msemaji wa wizara ya afya Nchini Palestina amesema kuwa
idadi kubwa ya wapalestina waliouwawa ama kujeruhiwa walikuwa wakiendesha
shughuli za ununuzi wa bidhaa.
Msemaji wa kundi la Hamas, linalothibiti maeneo hayo Sami
Abu Zuhri amekatalia mbali muafaka wa amani na kutaja kuwa hauna maana.
Wanahabari wanasema kuwa haijafahamika bayana iwapo
wapalestina walikuwa wakijua kuwa watashambuliwa.
Shambulizi Gaza laua watu 15
Walioshuhudia wanasema kuwa, waliona moshi
mkubwa ukifuka
kutoka eneo hilo huku magari ya kutoa huduma ya kwanza yakionekana yakiingia na
kutoka mahalipa tukio.
Aidha inasemekana kuwa mmoja wa waandishi habari ameuwawa
katika shambulio hilo.
Wakati huo huo, majeshi wa nchi kavu ya Israel
yamesema yatasitisha mapigano kwa muda wa masaa manne, lakini kauli hiyo
haitotumika katika maeneo ambako wanajeshi wake wanaendeleza operesheni.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment