Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paulo akionyesha moja ya silaha zilizokuwa zikitumika katika matukio ya ujambazi, ni baada ya kukamata majambazi wanne na kuwatia nguvuni.
WATU sita wanashikiliwa na polisi mkoani hapa , watatu kwa tuhuma za ujambazi na wengine wawili tuhuma za ujangili.Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonard Paulo aliwaambia waandishi wa habari jana , kukamatwa ka majambazi na majangili hao kumetokana na oparesheni maalumu iliofanywa na jeshi hilo.Kamanda huyo alisema kuanzia Juni 16 hadi Julai 3 mwaka huu jeshi hilo liliendesha oparesheni hiyo na kufanikikiwa kuwakamata waharifu hao na silaha mbalimbali.
Aliwataja majambzi hao Saidi Salehe (30) mkazi wa Kilosa, Alayazi Makweya (30) mkazi wa Ludewa na Abdul Mateo maarufu kama baba Ubaya mkazi wa Turiani Mvomero.
Alisema majambazi hao walikamatwa wakiwa na bunduki aina ya AK 47 ikiwa na
risasi 3 kinyume na sheria.
risasi 3 kinyume na sheria.
Hata hivyo kamanda huyo alisema Jeshi hilo pia lilifanikiwa kumtia nguvuni jambazi ambaye tayari aliwahi kufungwa miaka 10 kwa makosa ya ujambazi.
Kamanda huyo alisema jina la jambazi huyo lime hifadhiwa kwa sababu ya wanaendelea na uchunguzi zaidi na kwamba alikamatwa eneo la Mikumi wilayani Kilosa.
Kamanda huyo alisema Julai 16 mwaka huu jeshi hilo liliwakamata majangili wawili Ayoub Abeid maarufu Mkwenejele (36) mkazi wa Kilosa na Nassoro Mohamed maarufu kwa jina la Kambala.
Kamanda huyo alisema majangili hao walikamatwa katika eneo la Mzombe Tarafa ya Mikumi wilyani Kilosa baada ya polisi waliokuwa katika oparesheni hiyo kuwatilia mashaka watu hao walikuwa wamevalia makoti makubwa meusi.
Alisema watu hao walikuwa na pikipiki namba T 630 BVH SunLg na kamba baada ya kuwapekuwa wakuwakuta na silaha aina ya Riffle namba AO48441 na risasi 13 bila kibali cha kumuliki silaha hiyo.
Alisema vitu vingine walivyokutwa navyo majangili hao ni unga na samaki pamoja na mazni wa kupimia bidhaa ambao walikuwa wakiutumia kwa kupima wanyama hao baada ua kuwakamata.
Alisema watuhumiwa hao walipohojiwa walisema wamekuwa wakifanya shughuli ya kuwanda tembo na nyati na kwamba hata katika simu zao walikuwa wamehifadhi picha za wanyama hao.
No comments:
Post a Comment