Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi DAVID A. MISIME – SACP
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Moto mkubwa umetokea
katika eneo la Jamatini Manispaa ya Dodoma na kusababisha hasara ambayo thamani
yake bado haijafahamika.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi DAVID A. MISIME – SACP, amesema
kuwa mnamo tarehe 11/07/2014 majira ya 20:40hrs katika eneo la Jamatini Mkoa wa
Dodoma, kulitokea ajali ya moto ulioteketeza vibanda sitini na tatu (63) vya
wajasiliamali wadogowadogo ingawa hapakuwa na madhara yoyote kwa binadamu.
Chanzo cha moto huo
bado hakijafahamika na hakuna mtu anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana
na tukio hilo.
Aidha Jeahi la Polisi
Mkoa wa Dodoma wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuweza kubaini chanzo
cha moto huo.
Baadhi ya wajasiriamali wakiokoa mali zao
Kamanda wa Polisi
anawapa pole waliounguliwa na vibanda na kupoteza mali zao na kusema kuwa
inabidi kila mtu na mamlaka zote kuwa na mipango mizuri wanapojenga nyumba au
vibanda vya biashara kuhakikisha wanaacha nafasi ya magari ya huduma kama zima
moto kupita kwani katika tukio hili
kilichowapa ugumu Jeshi la zimamoto na Polisi kushindwa kuzima moto huo kwa haraka ni kutokana na waliojenga vibanda hivyo hawakuweka njia ya magari ya zima moto kuingia na kuzima moto huo. Tunaamini swala la mipango miji lingezingatiwa vibanda vingi pamoja na mali nyingi kiasi hicho hazingeteketea

No comments:
Post a Comment