Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa
man United Louis Van Gaal alithibitisha kwamba kuna kundi la wachezaji
litaondoka mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii.Leo hii zimetoka taarifa kwamba
kiungo wa kimataifa wa Japan, Shinji
Kagawa ni mmoja wa wachezaji wanaondoka
kwenye klabu hiyo kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili.Shinji anatarajiwa
kujiunga na klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa
£8m.
Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani leo hii tayari
kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake Dortmund.
Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu iliyopita kwa
ada ya uhamisho wa £12m.
No comments:
Post a Comment