Boss wa Manchester United Louis van Gaal anataka kumsajili
kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, kwa mkataba wa pauni milioni 34 kiasi
ambacho kitafikisha pauni milioni 200 za kununua wachezaji Old Trafford katika
kipindi cha miaka miwili (Independent), United huenda wakamtoa Javier
Hernandez, 26, kwenda Juventus, katika mkataba wa Vidal (Daily Express),
Manchester United pia wanatarajia kutaka kumsajili Daley Blind, 24 kutoka Ajax
kwa pauni milioni 18 katika siku chache zijazo
(Sun), Arsenal wanaonekana
kuzidiwa kete na Roma, kumsajili beki wa kati Kostas Manolas, 23 kutoka
Olympiakos (Goal), Manchester United na Arsenal wamepata matumaini ya kuendelea
kumfuatilia beki wa Roma Mehdi Benatia, 27, baada ya klabu hiyo ya Italia
kuvunja mazungumzo na Bayern Munich (Daily Star), Arsenal huenda wakamfuatilia
Danny Welbeck, 23, kutoka Man United, au Loic Remy, 27, kutoka QPR kuziba pengo
la Olivier Giroud ambaye huenda akakosa kucheza kwa miezi mitatu kutokana na
jeraha la kiwiko cha mguu (Daily Telegraph), Southampton wameanza kumfuatilia
beki wa Atletico Madrid Toby Alderweireld, 25, na kuwazidi Monaco (Times),
Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 8 kumchukua nahodha wa Sevilla
Federico Fazio, 27 (London Evening Standard) Chelsea wanazungumza na Roma
kumchukua Mattia Destro, 23 (Daily Mirror), QPR wanakaribia kumsajili beki wa
Liverpool Jack Robinson, 20 kwa mkataba wa pauni milioni 1 (Daily Mirror), West
Ham wamemuulizia beki wa kati wa Bayer Leverkusen Philipp Wollscheid, 25,
(Daily Mail), Sunderland, QPR na West Brom wanamtaka kiungo wa Leicester Andy
King, 25, (Sun), AC Milan bado wanataka kumchukua Fernando Torres kutoka
Chelsea, wakala wake akipendekeza kumchukua kwa mkopo, ingawa mshahara wake
mkubwa unaonekana kuwa kikwazo (Metro), Napoli wataanza kumfuatilia tena kiungo
wa Tottenham, Sandro kwa mkopo (The Times), Sporting wamewaambia Arsenal kuwa
watakubali kitita cha euro milioni 30 kumsajili William Carvalho, kama Arsenal
watakubali kumtoa Serge Gnabry, Francis Coquelin au Yaya Sanogo kwa mkopo (The
Times), Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o. Roberto
Martinez alikuwa akimtaka Danny Welbeck wa Man United, lakini alikatishwa tamaa
na bei ya Pauni milioni 15 (The Times) na boss wa Inter Milan, Walter Mazzarri
amewaambia watu wake kuwa wako huru kujaribu kumsajili Ezequiel Lavezzi kutoka
Paris St-Germain (Tuttosport). Zimesalia siku sita kabla ya dirisha la usajili
kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share hizi na wapenda soka wote.
Cheers!!
No comments:
Post a Comment