MWANAFUNZI wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani Mbarali, Mkoa
wa Mbeya, Vena Mtati (27) (pichani)
anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai mazito ya kumuua mtoto
wake kwa kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa rambo na kuutia ndani ya mfuko
wa salfeti kisha kuuficha
chini ya kitanda!
Tukio hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa
ikizingatiwa kuwa mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi,
lilijiri Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni, Kata ya
Mvinjeni mjini hapa.
SHUHUDA
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba
inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa
huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito. “Wiki mbili
zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce ambaye alikuwa
amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba kubwa, baada ya siku tano
tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho.
Kikaongeza: “Siku ya tukio, Joyce yeye ambaye ni mwenyeji
alitoka kwenda katika shughuli zake, akamuacha Vena akiwa chumbani. Nadhani
ndipo aliposhikwa na uchungu, akajifugua mtoto wa kike.
“Ilikuwa asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba
hicho. Zile kelele zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.
Akiwa chini ya ulinzi.
“Tuliposikiliza kwa
makini, mara sauti ya redio ikaongezwa ili kufanya kelele hizo zisisikike kwa
nje. Lakini kwa vile sisi majirani
tulijua kwamba ndani ya chumba kile kuna mjamzito na kelele alizopiga
mtoto si za kawaida ndipo tulipomtafuta mwandishi wa habari (hizi),” kilisema
chanzo hicho.
HATUA ZA HARAKA
Mwandishi wetu alipopatikana na kunyetishiwa kuhusu kuwepo
kwa uwezekano wa mama ambaye ni nesi kumuua mtoto wake aliyejifungua,
aliwasiliana na Polisi wa Dawati la Jinsia.
Polisi hao, awali
walimtafuta mwenyeji wa mtuhumiwa huyo, yaani Joyce ambaye alikuwa kwenye mihangaiko yake.
Alipopatikana
alipokonywa simu yake ya mkononi ili asiweze kuwasiliana na mtuhumiwa.
Aliulizwa kama ana
mgeni nyumbani kwake, akakiri. Akaulizwa kama mgeni huyo amejifungua, akakataa
ndipo wakamchukua kwenda naye nyumbani kwake kumfuata mtuhumiwa huyo.
ASKARI WAFIKA ENEO LA TUKIO
Paparazi wetu akiwa ameongozana na askari hao walifika
kwenye chumba hicho na kumkuta Vena akiwa amesimama mlangoni.
Alipoulizwa kama
amejifungua, awali alikataa katakata lakini baada ya kubanwa na kutishiwa kuswekwa ndani, alikiri
kujifungua na kusema kwamba mtoto huyo amemficha uvunguni mwa kitanda.
Denti (aliyeshika kiroba chenye mwili) akiwa chini ya ulinzi
wa polisi (Kulia) ni mwenyeji wake, Joyce.
DAMU SAKAFUNI
Ndani ya chumba hicho, sakafuni kulikuwa na damu zilizodaiwa kumtoka mtuhumiwa huyo wakati
akijifungua mwenyewe!
POLISI WAPEKUA UVUNGUNI
Polisi walizama chumbani, wakainama kuchungulia chini ya
kitanda. Walichoanza kukiona ni mfuko wa salfeti, wakauvuta kuutoa. Walipofungua ndani, wakakuta mfuko wa
rambo, wakaingiza mkono na kutoa kifurushi kikiwa kimeviringishwa nguo nyingi
na ndiye mtoto huyo alimohifadhiwa.
HEBU SOMA HII, INAUMA ZAIDI
Mbali na mwili wa mtoto huyo kuviringishwa nguo hizo, pia
ulimwagiwa chumvi na vumbi la mkaa ambapo ilidaiwa mtuhumiwa alifanya hivyo ili
mwili huo usitoe harufu utakapotupwa porini.
Majirani walisema maarifa hayo, mtuhumiwa aliyapata kwa
sababu tayari anajua namna ya kuhifadhi mwili wa mwanadamu, kwa mwanamke asiye
na ujuzi asingeweza kufanya hivyo.
Vena Mtati akiwa na kiroba hicho.
SABABU YA MTOTO
KUUAWA
Kuna madai kwamba, mtuhumiwa huyo aliwaambia polisi kuwa
alifikia uamuzi wa kumuua mtoto huyo kufuatia mwanaume aliyempa ujauzito
aishiye jijini Dar es Salaam kumuahidi ndoa lakini akaingia mitini.
ORODHA YA WALIOKAMATWA
Baada ya polisi kusikiliza maelezo ya mtuhumiwa huyo,
walimkamata yeye, mwenyeji wake Joyce na mmiliki wa nyumba hiyo ambaye jina
halikupatikana mara moja.
Polisi walisema mmiliki wa nyumba hiyo alikamatwa kwa sababu
alikiuka sheria za mji ambapo alitakiwa kutoa taarifa za kumpokea mgeni huyo
kwenye serikali za mitaa lakini hakufanya hivyo huku Joyce akidaiwa kutambua
kuwa mgeni wake alijifungua lakini akawaambia hakujifungua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment