Madaktari wawili, Hamis Chacha (kushoto) na Shengena
wanaotuhumiwa kwa jaribio la utoaji mimba.
IMEBUMA kwao! Madaktari wawili, Hamis Chacha na Shengena wa
zahanati moja iliyopo Yombo Buza jijini Dar wamejikuta katika wakati mgumu
baada ya polisi kuwaibukia na kuwaweka chini ya ulinzi kwa madai ya kufanya jaribio la kumchoropoa mimba msichana
mmoja aliyedaiwa kuwa ni denti wa chuo f’lani cha
digrii za juu, Dar.
Tukio hilo la aina yake lilijiri hivi karibuni, mwaka huu
katika zahanati hiyo ambayo jina tunalihifadhi kwa sasa.Awali, Operesheni
Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global
Publishers ikiwa katika pitapita zake
ilinasa tukio hilo ambapo polisi walikuwa ndani ya zahanati hiyo wakiwaweka chini
ya ulinzi madaktari hao.
OFM ilifanikiwa kuzama ndani ya zahanati hiyo na kuingia
kwenye chumba cha kilichodaiwa hutumika katika zoezi hilo.
No comments:
Post a Comment