Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 21, 2014

Top 10 ya wachezaji wanaolipwa zaidi Ligi kuu ya Tanzania Bara Jaja amfunika Okwi

 Mshambuliaji mpya wa Yanga, Geilson Santos ‘Jaja’.
Na Mwandishi Wetu MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Geilson Santos ‘Jaja’, amempiku kwa mara nyingine mshambuliaji mpya wa Simba, Emmanuel Okwi, safari hii ikiwa ni katika mshahara wa mwezi.Siku chache zilizopita, Jaja amekuwa ndiye mchezaji gumzo zaidi hasa baada ya kufunga mabao mawili wakati Yanga ilipoivaa Azam FC na kuitwanga kwa mabao 3-0 kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.


Umaarufu huo wa Jaja ulifanya amfunike Okwi huku mashabiki wa Yanga wakiona wamepata mbadala wa kuwapoza baada ya Okwi kurejea Simba, ghafla.
Kwa mara nyingine, Jaja amezidi kung’ara baada ya mshahara wake anaochota kwa mwezi Yanga kuwa unazidi ule wa Okwi kwa dola 100 (Sh 168,000).





No comments:

Post a Comment