Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 16, 2014

TRAFIKI ALIYEGONGWA NA DALADALA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI

Hali ya Askari wa usalama barabarani, aliyejulikana kwa jina la Riziki, WP 2806 Cpl Riziki, aliyegongwa na daladala aina ya DCM wakati akiwa katika harakati za kutimiza majukumu ya kazi eneo la Mbagala Rangi Tatu, hali yake inaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa Askari ambaye hakupenda jina lake litajwe aliiambia Blog hii kuwa afande huyo anapatiwa matibabu hospitali ya Muhimbili na hali yake inaendelea vizuri.

"Mimi nimetoka kumjulia hali, kwakweli alikuwa amepoteza fahamu ila kwasasa anaendelea vizuri maana alikuwa ameshazinduka,"alisisitiza Askari huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe
Na KajunasonBlog 

No comments:

Post a Comment