Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, October 17, 2014

ALIYEMUAA AFISA USALAMA WA TAIFA NAYE AUAWA NA POLISI JIJINI DAR


Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amethibitisha kuwa Jeshi lake limefanikiwa kumkamata jambazi sugu aitwaye Paulo Thamas Milanzi maarufu Chinga (35), Mmakonde mkazi wa Chanika.
Amesema baada ya majibizano ya risasi jambazi hilo lilijeruhiwa na kufikishwa hospitali ya Muhimbili kwa matibabu lakini baadaye alifariki dunia.
Alisema jambazi huyo lilikuwa akitafutwa na polisi

 
kutokana kuhusika kwenye matukio ya mauaji na wizi ikiwemo tukio la kuuawa kwa Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Taifa, Sylivabus Adrian Mzeru Aprili 29, 2014 liliotokea Uwanja wa Ndege.


Aliongeza kuwa Chinga alikamatwa na bastola aina ya Star.'


Majambazi wenzake walikamatwa na kwa sasa wako gerezani wakisubiri taratibu za kisheria kuchukua mkondo wake.

No comments:

Post a Comment