Caine Hutchings akipendekeza kwa Emily Dukeson nia ya kutaka
kuoana naye muda mfupi baada ya gari lake kugonga mti.Emily alikubali.
Caine Hutchings alipendekeza kwa Emily Dukeson nia ya kutaka
kuoana naye muda mfupi baada ya gari lake kugonga mti.
Mwanamke alikubali pendekezo hilo la kuoana wakiwa katika
gari la polisi wakifuatilia ajali ya barabarani.
Caine Hutchings alipendekeza kwa Emily Dukeson nia
ya kutaka
kuoana naye muda mfupi baada ya gari lake kugonga mti, wakielekea ufukweni mwa
bahari ambapo awali alipanga kutoa pendekezo hilo.
Badala yake, wapenzi hao kutoka Radstock walikubaliana
kufunga ndoa wakati wakiendeshwa kutoka eneo la tukio.
Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa katika ajali ya Jumamosi
karibu na Shapwick katika barabara ya A39 na hakuna faini iliyotozwa kutokana
na ajali hiyo.
Bwana Hutchings, mwenye umri wa miaka 30, amesema:
"Tulikuwa tu katika gari la polisi muda mfupi lakini ajali imefichua kila
kitu, kwa hiyo niliamua kuwa nitatoa pendekezo langu hapo na kwa sababu lolote
linaweza kubadili hali hiyo katika muda mfupi na sikutaka kusubiri zaidi.
"Tulipiga picha ya mimi nikipiga goti moja chini mbele ya gari la polisi
baada ya kwenda katika mkahawa au hakuna mtu anayeweza kuamini
nilichofanya."
Bi Dukeson, mwenye umri wa miaka 27, amesema: "Sikuwa
na wazo kwamba hilo litatokea. Lakini kwa namna ninavyofahamu tulikuwa
tunakwenda Blue Anchor kuwachukua mbwa kwenda matembezini.
"Katika gari Caine aliuliza 'hivi kweli unafikiri
tunakwenda mwendo wote huu ni kwa ajili ya kuwatembeza mbwa tu? na alivuta kikasha
chenye pete.
PC Nicola Rickards, ambaye alikuwa akiendesha gari la
polisi, alisema: "Ghafla alitoa kikasha katikati ya safari. Sina uhakika
nani alifurahi zaidi."
Wapenzi hao wamesema walikuwa wanapanga kuoana mwaka ujao.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment