Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, zinasema
kuwa idadi kubwa ya wanawake wengine wametekwa nyara na kundi la wapiganaji la
Boko Haram.
Wiki jana maafisa wakuu wa nchi hiyo walitangaza kuafikia
makubaliano ya kusitisha vita na kundi hilo.
Kwa hiyo kundi hilo lilikubali kuwaachilia wasichana zaidi
ya miambli waliotekwa na kundi hilo kama
sehemu ya makubaliano hayo miezi sita
iliyopita.
Kulingana na taarifa kutoka kwa wakazi wa eneo hilo,
wapiganaji wa Boko Haram walishambulia vijiji viwili katika jimbo la Adamawa -
Waga Mangoro na Garta.
Kisha wakawateka wasichana na wanawake wengi.
Vijini hivi vinapakana na miji ya Madagali na Michika ambayo
imekuwa chini ya udhibiti wa wapiganaji hao kwa wiki kadhaa.
Kundi la kwanza la wasichana wlaiotekwa nyara na Boko Haram
ambao bado kuachiliwa
Mashambulizi hayo yalifanyika Jumamosi siku moja tu baada ya
jeshi la Nigeria kutangaza makubaliano ya kusitisha vita yameafikiwa na Boko
Haram.
Kama sehemu ya makubaliano hayo, serikali ilisema wasichana
219 waliotekwa kutoka Chibok mwezi Aprili, wataachiliwa hivi karibuni.
Tangu tangazo hilo kutolewa, kundi hilo limeendelea kufanya
mashambulizi, na hapajakuwa na kauli yoyote ikiwa wasichana wa Chibok
wameachiliwa.
Kulingana na serikali, mazunguzmo yalitarajiwa kufanyika
kati ya serikali na Boko Hara, wiki hii nchini Chad.
Wakati huohuo, polisi wanasema kuwa shambulizi lililofanywa
katika jimbo la Bauchi liliwaua watu 5.
Licha ya kwamba mashambulizi yoyote yanayofanywa kaskazini
mwa Nigeria hulaumiwa kwa Boko Haram, kundi hilo huwa kwa kawaida halijibu
haraka na kwa hivyo huwa vigumu kuthibitisha kweli ikiwa ni wapiganaji hao
waliofanya mashambulizi hayo.
No comments:
Post a Comment