FC Barcelona jana usiku ilicheza mechi yake ya 7 katika ligi
kuu ya Hispania bila kupoteza mchezo wowote, wakishinda mechi 6 na kutoa sare
moja.
Lionel Messi alifunga goli lake 402 tangu aanze kucheza soka
la ushindani na baadae akamtengenezea Neymar aliyehitimisha ushindi wa 2-0
dhidi ya Rayo Vallecano.
Kutokana na ushindi huo kikosi cha Luis Enrique sasa
kimefanikiwa kuwa timu ya kwanza katika historia ya La liga kucheza mechi 7 za
mwanzoni mwa ligi hiyo bila kuruhusu wavu wao kugushwa.
Pia wakati huo huo golikipa wa timu hiyo, Mchile Claudio
Bravo ameweka rekodi mpya ya katika kulinda lango lake.
Bravo amevunja rekodi ya kucheza dakika nyingi bila kuruhusu
wavu wake kuguswa, mpaka kufikia sasa Bravo amecheza jumla ya dakika 561 bila kufungwa
goli, akivunja rekodi ya golikipa wa zamani wa Barca, Pedro Artola aliyecheza
kwa dakika 560 bila kufungwa goli katika msimu wa 1977-78.
No comments:
Post a Comment