Ikiwa ni siku chache tu zimebakia ili shangwe za Serengeti
Fiesta zitawale katika maskio ya wakazi wa Dar es Salaam, October 18, Meneja wa
T.I., Jason Geter pamoja na meneja wa Wizkid na Waje, Cecil Hammond, wanatarajia
kutoa semina kwa wadau wa muziki itakayofanyika ijumaa hii. Akizungumza Mtandao
huu leo
mwenyekiti wa tamasha la Serengeti Fiesta 2014,
Sebastian
Maganga, amesema meneja wa T.I. na yule wa Waje wanatarajia kuingia Jumatano,
October 15 ili kujiandaa na shughuli mbalimbali ikiwemo semina pamoja na
kufungua duka litakalouza kazi za T.I.
“Mpaka sasa ratiba inaenda vizuri, meneja wa T.I ‘Jason
Geter’ na meneja wa Waje na Patoraking, wanatajia kuingia usiku wa Jumatano,
kwa sababu kama meneja wa T.I. anakuja mapema ili kuangalia mazingira na
atakuwa na semina na wadau wa muziki kuzungumzia jinsi muziki au msanii
unavyoweza kutumia jina lako kibiashara. Pia atafungua duka ambalo litakuwa
linauza productiob za T.I. Pia meneja wa Waje ‘Cecil Hammond’ atakuwepo kwenye
semina hiyo,” alisema Sebastian Maganga.
Cecil Hammond
Pia Sebastian alisema wasanii wa kimataifa wanaotarajia
kupagawisha kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta ni T.I, kutoka Marekani, Waje na
Patoraking kutoka Nigeria pamoja na Victoria Kimani kutoka Kenya. Pia amedai
kuna msaani mmoja mkubwa kutoka Nigeria ambaye bado wapo kwenye mazungumzo na
jibu ramsi litapatikana kesho mchana.
“Katika wasanii wa kimataifa T.I. ataingia Dar Ijumaa
usiku,” amesema.
Wasanii wa Bongo wanaotarajia kupanda jukwaa moja na wakali
hao kutoka nje ni, Diamond, Alikiba, Ommy Dimpoz, Mr Blue, Stamina, Nay wa
Mitego, Vanessa Mdee, Mwana FA, Weusi,Young Killer Msodoki, Linah Sanga, Recho,
Barakah Da Prince, Mo Music, pamoja na Super Nyota G.Luck, K. Style pamoja na
Edu Boy.
CDT:BONGO 5
No comments:
Post a Comment