Picha za waandamanaji wakielekea kituo cha polisi.
KAMERA ya GPL imewashuhudia wakazi wa Kunduchi jijini Dar es
Salaam, wakiandamana kuelekea vituo vya Polisi vya Wazo na Mtongani, baada ya
kudai kuwa ndugu zao wamekamatwa wakiwa hawana makosa na kupelekwa kituoni.
Wakizungumza na GPL baadhi ya waandamanaji walisema difenda
tano za Polisi zilikwenda eneo hilo na kuanza kukamata watu ovyo kwa madai kuwa
ni wahuni na wavuta bangi.
Dereva mmoja wa bodaboda alisema kawaida ya Polisi hao
hufika na kuwakamata wahuni, wavuta bangi na vijana walio katika makundi ya
uhalifu, ila kilichotokea ni wahuni hao kushtuka na kukimbia, ndipo polisi
wakaaanza kukamata watu hovyo hata wasiohusika.
(Habari/Picha na:
Gabriel Ng’osha/GPL)
No comments:
Post a Comment