Jeshi
la Polisi kikosi cha wanamaji limekamata jahazi moja ambalo linatoka
nchini Irani ambalo linadaiwa kuwa na shehena ya dawa za kulevya.
Akizungumza kuhusu tukio hilo kamanda wa kikosi hicho kamanda Mboje Kanga
amesema walilikamata jahazi hilo baada ya kulitilia shaka na ndani yake
wapo watu.
Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha kuzuia na kupambana na dawa
za kuleya nchini Godfrey Nzowa amesema mapambano bado yanaendelea japo
zipo changamoto nyingi na kuongeza kuwa robo tatu ya vigogo wa dawa za
kulevya wamekwisha kamatwa.
No comments:
Post a Comment