Wayne Rooney yuko 'fiti' na ataanza kwa upande wa Manchester
United dhidi ya Manchester City, lakini mshambuliaji Radamel Falcao hatocheza
kutokana na kuwa bado majeruhi.
Meneja wa Man Utd Louis van Gaal amethibitisha kuwa nahodha
wake atacheza baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake, na kusema taarifa
zinazodai kuwa ameumia si za ukweli.
Falcao hakucheza katika mechi dhidi ya Chelsea iliyomalizika
kwa sare ya 1-1.
Winga Antonio Valencia naye amerejea baada ya kupona msuli
wa paja.
Van Gaal ametupilia mbali taarifa zilizodai kuwa Rooney hana
uhakika wa kucheza kwa sababu alionekana akichechemea katika shughuli moja ya
wadhamini siku ya Jumatatu, Old Trafford.
No comments:
Post a Comment