Bilionea Mharami akiwa na wahalifu wenzake wanne chini ya
ulinzi mkali ndani ya Mahakama ya Kisutu. (Picha na Maktaba yetu)
KESI inayomkabili mfanyabiashara bilionea jijini Dar,
Mharami Mohamed Abadallah ‘Chonji’ (44) anayedaiwa kukutwa na madawa ya kulevya
‘unga’ aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 300,000,000 imetajwa leo katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar na kuahirishwa mpaka Novemba 19, mwaka huu
itakaposikilizwa tena.
Chonji amefikishwa mbele ya Hakimu Janeth Kaluyenda sambamba
na Rehani Mursal (45), mkazi wa Mburahati (Dar), Abdul Abdallah (37), mkazi wa Mbezi
Shamba (Dar), Tanaka Mwakasaburi (35), mkazi wa Magomeni- Makanya (Dar) na
Maliki Zuberi (29), mkazi wa Magomeni Mwembechai (Dar).
No comments:
Post a Comment