NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar,
Salum Mwalimu, amewasihi wakazi wa Jiji la Mbeya kuendelea kukiunga mkono Chama
hicho katika chaguzi zijazo ili waweze kushika dola.
Mwalimu alitoa wito huo jana alipokuwa
akihutubia mamia ya Wafuasi wa Chama hicho katika mkutano wa hadhara
uliofanyika Iyela Airport ya zamani jijini Mbeya.
Alisema ni vema wananchi wakalinganisha
maendeleo waliyoyapata baada ya eneo lao kuongozwa na Chadema na kabla ya
hapo kisha wakatoa uamuzi sahihi katika chaguzi zijazo kwa kuendelea kukipa
majimbo Chama hicho.
Mwalimu alisema Majimbo mengi ambayo
Chadema inawabunge wake hali ya maendeleo inaenda kwa kasi kubwa sana tofauti
na awali ambapo majimbo hayo yalishikiliwa na CCM na kuongeza maeneo mengi
ukusanyaji wa mapato umeongezeka kwa Wabunge hao kudhibiti mianya ya
Halmashauri kuchakachua mapato.
Alitolea mfano Majimbo ya Mbeya mjini,
Momba,Iringa Mjini, Mwanza na Arusha ambako alisema hakuna vitega uchumi
vilivyoongezeka kabla ya uchaguzi na baada ua uchaguzi lakini ukusanyaji wa
mapato ya Halmashauri yanaongezeka kwa kasi kubwa.
Naye Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya
Mbeya Mjini, John Mwambigija alisema Chama chake kimejipanga kuhakikisha kinachukua
mitaa yote 181 ya Jiji la Mbeya katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
unaotarajiwa kufanyika Disemba mwaka huu.
Mwambingija alisema wamejipanga kuchukua
mitaa yote kwa kuwahamasisha wanachama wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha
katika daftari la kupigia kura ili siku ya uchaguzi wanachama wengi wawe na
sifa ya kupiga kura.
Alisema vijana ndio wanapaswa kujitokeza
kujiandikisha siku za mwanzo ili kuwazidi kete wapinzani wao ambao ni Chama cha
Mapinduzi na kusisitiza kuwa siku ya kujiandikisha hata vijana wadogo chini ya
miaka 18 ni vema wakatumia mwanya wa kudanganya umri ili waweze kupata idadi
kubwa ya wanachama.
Aliongeza kuwa mikakati mingine tayari
Chama kimewaandaa walinzi wake Red Brigedi kuhakikisha siku ya uchaguzi
wanalinda maboksi ya kupigia kura ili kuepuka udanganyifu wowote unaoweza
kujitokeza kwa wasimamizi wa uchaguzi.
Mwambigija alisema Redbrigedi wamepewa
mafunzo maalumu ya kupambana na udanganyifu wowote kwa kuweza kuwadhibiti
watendaji wa Mitaa watakaosimamia uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuwaadhibu kwa
vipigo kama itabainika.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment