WIKI iliyopita tuliwaletea marais waliouawa kwa risasi
wakiwa madarakani. Wiki hii tunawaletea wabunge wa Tanzania waliokufa kwa
ajali, iwe ndege, gari au usafiri wowote ule!
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime (Chadema), marehemu
Chacha Zakayo Wangwe enzi za uhai wake.
Hussein Ramadhan Shekilango; alikuwa Mbunge wa Jimbo la
Korogwe (CCM) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (utawala). Alifariki dunia
Mei 11, 1980 kwa ajali ya ndege iliyotokea kwenye milima ya Arusha. Kumuenzi,
serikali iliipa jina Barabara ya Shekilango iliyopo Sinza, Dar.
Juma Jamaldin Akukweti; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tunduru
(CCM) na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge). Alifariki Januari 4, 2007
Hospitali ya Johannesburg, siku chache baada ya ajali ya ndege iliyoanguka
ikitaka kupaa Desemba 16, 2006 jijini Mbeya alikokuwa kwa shughuli za kikazi.
Aliyekuwa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini,
Zanzibar, Mussa Khamis Silima enzi za uhai wake.
Chacha Zakayo Wangwe; alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime
(Chadema). Alifariki dunia papo hapo kwa ajali mbaya ya gari dogo aina ya
Toyota Corolla iliyotokea maeneo ya Kongwa, Dodoma, saa 2: 55 usiku wa Julai
27, 2008 akiwa njiani kuelekea msibani Dar.
Salome Joseph Mbatia; alikuwa Mbunge wa Viti Maalum-CCM na
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto. Alifariki papo hapo Oktoba
23, 2010 katika ajali mbaya ya gari lake aina ya Nissan Patrol kugongana uso
kwa uso na Fusso maeneo ya Kibena, akiwa njiani kwenda Njombe.
Aliyekuwa
Mbunge wa Viti Maalum-CCM na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na
Watoto, Salome Joseph Mbatia enzi za uhai wake
Regia Estelatus Mtema; alikuwa Mbuge wa Viti Maalum
(Chadema). Alifariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Toyota Land Cruiser
iliyotokea maeneo ya Ruvu Darajani, Mkoa wa Pwani Januari 14, 2012 akiwa njiani
kutoka Dar kwenda Ifakara kukagua kiwanja alichopewa na wazazi wake.
Mussa Khamis Silima; alikuwa Mbunge wa Baraza la Wawakilishi
Jimbo la Uzini, Zanzibar. Alifariki katika ajali ya gari Agosti 23, 2011 maeneo
ya Nzuguni, Dodoma pamoja na mkewe, Mwanaheri Fahari. Marehemu alikuwa
akielekea bungeni Dodoma kutokea Dar.
Aliyekuwa Mbuge wa Viti Maalum (Chadema), Regia Estelatus
Mtema enzi za uhai wake.
Edward Moringe Sokoine; alikuwa Mbunge wa Jimbo la
Monduli (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania. Alifariki kwa
ajali Aprili 12, 1984 eneo la Dumila, Morogoro. Ili kumuenzi, serikali imetoa
jina la Barabara ya Sokoine, ipo Posta jijini Dar na Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine, Morogoro.Chanzo GPL
No comments:
Post a Comment