Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, December 30, 2014

MKAZI WA KIJIJI CHA KIBARA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUTENGENEZA NOTI BANDIA.


Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kibara wilayani Bunda mkoani Mara Jonathani Daniel (33) kwa tuhuma za  kupatikana na noti bandia 75, za shilingi elfu kumi kila moja zenye thamani ya shilingi 750,000, pamoja na vifaa vya kutengenezea pesa hizo bandia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa  kwa vyombo vya habari na  kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea Desemba 27 mwaka huu,majira ya saa 2:00 usiku katika eneo la kituo cha basi kwenye kijiji na kata ya Kakola  tafara  ya Msalala wilayani Kahama.
Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wa jeshi hilo wakati wakiwa katika doria ya kawaida kwenye kituo hicho cha mabasi akiwa na noti hizo bandia na kuwa kati yake noti 3 zina namba BL, 0315207, noti (32) BB 0315203, noti (21) BE 0315206 ,  na noti (19) zikiwa na namba BC 0315209.

Kamanda Kamugisha ameongeza kuwa licha ya kumkamata mtuhumiwa na noti hizo  bandia, pia amekamatwa akiwa na  bando ya karatasi , Sindano pamoja na chupa  ya konyagi iliyokuwa na unga mweupe, vifaa ambavyo vinasadikiwa kutengenezea noti hizo.
Aidha kamanda Kamugisha ameongeza kuwa Mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazo mkabili mara baada ya upelelezi wa jeshi hilo kukamilika.


CHANZO: ITV TANZANIA

No comments:

Post a Comment