Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 20, 2014

UJUMBE WA TTB, TANAPA UKIONGOZWA NA MHE. ABDULKARIM SHAH WAKARIBISHWA CHAKULA CHA JIONI UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC


 Mhe. Abdulkarim Shah Mbunge wa Mafya kwa tiketi ya CCM akiongozana na ujumbe wake wa Tanzania Tourist Board (TTB) na Tanzania National Parks (TANAPA) walipowasili Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Washington, DC kwenye chakula cha jioni walipokaribishwa Ubalozini hapo siku ya Alhamisi June 19, 2014. Wengine waliokaribishwa ni Jumuiya ya Watanzania DMV, Kamati ya maandalizi ya sherehe ya Vijimambo, Katibu wa Jumuiya New York alikuwepo lakini chini ya kivuli cha Miss Tanzania USA Pagent chini ya Ma Winny Case. Ujumbe wa TTB na TANAPA ulialianzia New York na wapo nchini Marekani kwa ajili ya kutangaza Utalii wa Tanzania kwa kufanya mazungumuzo na watu mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kwa ajili ya matangazo na kupata mbinu mbalimbali za kupambana na ujangili wa mali asili na hatimae kuutokomeza kabisa. Mjini New York walipata fulsa ya kufanya mazungumuzo na CNN International na Local na vyombo vingine vya habari yakiwemo magazeti kwa ajili ya kutangaza utalii na mali asili kitu ambacho kinaendelea pia kufanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Mhe. Liberata Mulamula na kufanya nchi ya Marekani kuongoza hivi sasa katika kupeleka watalii wengi nchini Tanzania. Katika picha Mhe. Abdulkarim akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly.
 Mkurugenzi mkuu wa Tanzania National Parks (TANAPA) Bwn. Allan Kijazi akisalimia na mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Ulotu wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington, DC.
Mkurugenzi masoko wa Tanzania Tourist Board (TTB) Bi. Teddy Mapunda akisalimiana na  mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Ulotu wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliopokaribishwa chakula cha jioni na Ubalozi wa Tanzania , Washington, DC. Nyuma ya Bi. Teddy Mapunda ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Tourist Board Bi. Devota Mdachi akisalimiana na Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Colonel Adolph Mutta.
 
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akifanya utambulisho wa wageni na maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na baadae kuwakaribisha chakula cha jioni.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akijipatia chakula, wengine katika picha ni Mariam Mkama, Edward Taji, Afisa Suleiman Saleh, Mercy Dachi na Rose Mzirai Commodore

RAIS KIKWETE ATOA MHADHARA KATIKA CHUO CHA ULINZI JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekumbuka enzi za kuwa mwalimu katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Monduli, Arusha, alipotoa  mhadhara  kuhusu Fursa (A lecture of Opportunity) katika Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo. Pichani anaonekana  Rais Kikwete akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wanafunzi hao baada ya mhadhara wake.
  Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amekumbuka enzi za kuwa mwalimu katika Chuo cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania cha Monduli, Arusha, alipotoa  mhadhara  kuhusu Fursa (A lecture of Opportunity) katika Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo. Pichani anaonekana  Rais Kikwete akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wanafunzi hao baada ya mhadhara wake. Pichani Rais Kikwete akijibu maswali kutoka kwa wanafunzi baada ya mhadhara wake
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wahadhiri na wanafunzi wa  Chuo cha Taifa cha ulinzi (National Defence College -NDC- ) kilichopo Kunduchi  jijini Dar es salaam ambako aliahidi kwamba baada ya kustaafu Urais mwakani atakuwa mwalimu chuoni hapo.
(PICHA NA IKULU)

WATU WATATU WATIWA MBARONI MKOANI PWANI,WAKUTWA NA BASTOLA NA SARE ZA JESHI


 Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei akionyesha silaha na mavazi ya kijeshi waliyokamatwa nayo Watuhumiwa hao.

Na John Gagarini, Kibaha

JESHI la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kuwakamata watu watatu akiwemo mtu Daniel Mtalisi mkazi wa Kisemvule wilaya ya Mkuranga ambaye alipitia mafunzo ya kijeshi kwa tuhuma za kufanya tukio la uhalifu wa kupora silaha na vitu mbalimbali.

Mtuhumiwa huyo ambayealiwahi kupata mafunzo ya kijeshi kwenye Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi namba 833 Oljoro Arusha na namba yake ni MT. 95150.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa waandishi wa habari mjini Kibaha, kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 17 mwaka huu majira ya saa 2 usiku huko Kijiji cha Kisemvule kata ya Vikindu kata ya Mkuranga wilaya ya Mkuranga.

MEYA WA ILALA MH JERRY SILAA ATEMBELEA NA KUKAGUA BARABARA YA TABATA-ST MARY'S YENYE MGOGORO BAINA YA MKANDARASI NA DAWASCO

 Meya Wa Manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa Wa Kwanza kulia  akifika eneo la Tabata St Marrys kukagua kipande cha barabara huyo ambacho kimezua mgogoro baina na Manispaa na Shirika la maji safi na salama DAWASA.
 Mwenyekiti wa Serikali za Mitaaa Bwana Hassan Chambuso akimuongoza Mh Meya wa manispaa ya Ilala Jery Silaa kwenda kujionea eneo la kipande cha barabara ya St Marys Tabata ambacho kinaleta shida baina ya Mkandarasi na Dawasa
Mkandarasi wa barabara ya Tabata-St Mary Bwana  George Lupia wa pili kutoka kushoto akitoa ufafanuzi kwa Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kuhusu kukwama kwake kuendelea na Ujenzi kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita Katikati ya barabara Hiyo.
Meya wa Ilala Mh Jery Silaa akifafanua Jambo kwa Mwenyekiti wa mitaa ya Tabata Bwana Chambuso kuhusu yeye Kulifuatilia Swala hilo kwenye mamlaka husika haraka iwezekanavyo,Pembeni yake ni Diwani wa Kata ya  Tabata St Marys Bi Mtumwa Mohamed mwenye Dira.
Mkandarasi Geoge Lupia Akimwelezea Meya wa Ilala Mh Jery Silaa kwamba wametumia pesa nyingi katika kuchimba eneo hilo na kupata usawa wa Barabara lakini kikwazo kimekuja baada ya kukuta mabomba ya Dawasa ambayo yamekatiza katikati ya barabara na pembeni Hivyo kuleta ugumu katika kufanikisha Umaliziaji wake.
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda Akimwelezea Meya Jerry Silaa kwamba washaongea na Dawasa lakini hawapewi ushirikiano wa kutosha na wa haraka katika kushughulikia utoaji wa Mabomba hayo
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda akiendelea kufafanua jambo kwa Mh Meya wa Ilala Jerry Silaa
Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa Akiongea na vyombo vya habari kutoa ufafanuzi wa nini kitafanyika ili kutatua mgogoro huo.

SKYLIGHT BAND YAZIDI KUKUBALIKA NA MASHABIKI, LEO KUZINDUA WIMBO WAO MPYA "PASUA TWENDE" NDANI YAK IOTA CHA THAI VILLAGE‏


Vijana machachari wa Skylight Band Kutoka kushoto Donode, Digna Mbepera, Sony Masamba na Mary Lucos wakitoa Burudani kwa mashabiki wao ndani ya Thai Village,USikose Leo kutakuwa pia na Uzinduzi wa Wimbo wao mpya PASUA TWENDE Itakuwa hapatoshiii.
Weweeee Usicheze na Sony masamba(katikati)akiyarudi mauno safi kabisaaaa kuwapa burudani wapenzi wa Skylight ndani ya Thai Village.
Hapo hapooo Taratibuuuu weweee Sam Mapenzi akiyarudi mastep ndani ya Thai Village Sony Masamba akifuahiii na Mashabiki Wake.
Sony Masamba (Mutoto ya kongo)akiporomosha Vocal Kali Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha Thai Village.
Kijana mdogo lakini mwenye Vocal kali : Hashim Donode akiimba kwa hisia kali kabisaaaa Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha maraha Thai village Sogea leo upate nyimboo kali pamoja na Uzinduzi wa Wimbo wao mpya.
Digna Mbepera (katikati)akifurahiii kwa staili kaliii za kuzungusha zungusha kwenye steji.
Hatariiiii hebu yaone majembe ya Skylight Band wakiongozwa na Joniko Flower(kushoto)Sony Masamba(katikati)na Sam mapenzi wakicheza sebene kaliiii za nguvuuu.
Hahahhaah Hapo sasaaaa hebu ona uchezaji wa staili hizooo ni Shidarrrrrrrrr
Sasa Hebu Tazama Iyo Video Hapo Chiniii Uamini ninachokuelezea Kutoka kwa Vijana Hawa mahiri wa Skylight Band.
DSC_0073
Daudi Tumba akifanya yake kwenye Tumba zake.
DSC_0085
Mpiga kinanda mahiri wa Skylight Band akikung'uta nota za kinanda ipasavyooo,Kwa mbaliii mzee wa drums Idrisa akizicharangaaaa drums zakeee.
DSC_0096
Mpiga Solo Gitaaa Allen Kisso akicharaza nyuzi zake 6 kwa Umahiri mkubwa kabisaa yani Rahaaa sanaaaa ukiwa unapewa burudani na Vijana hawa Ndani ya Thai Village
DSC_0160
Mpiga Bass Gitaa wa Skylight Band Tophy bass akilisukuma gita lake kwa umahiri kabisa.
Huyo ni Sam Mapenzi bwana au Tamu ya warembo akitoa vocal Kaliiiii kwa mashabiki wake.
Hahahahah Back Stage Napo Paliwaka Motoooooo wakati Donode na kampani yake wakiyarudi Mangoma kwa raha zaooooo.
DSC_0150
Huyo anaitwa Dr. Sebastian Ndege (Jembe ni Jembe) Mmiliki wa Bendi ya Skylight akimpa maelekezo kijana wake Sam Mapenzi kuhusiana na Uzinduzi wa wimbo wao mpya Ijumaa ya Leo Ndani ya Thai Village Usikoseeeeee.
Haya Sasa mashabiki haoooo wakipata kitu roho inapenda
DSC_0083
Heehehehehe Ayeeeee Ayeeeeeeeee mashabiki wakiimba wimbo wa Davido sambamba na Vijana wa Skylight Band (hawapo pichani)

TAZAMA PICHA ZA MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA

PG4A2995Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Wazee Mohammed Cheupe (katikati) na Seif Membe (kulia)  kutoka Jimbo la   Ruangwa ambao walitembela bunge mjini Dodoma Juni 20, 2014, kwa mwaliko wa mbunge wao Kassim Majaliwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PG4A3018Mbunge wa  Rungwe Magharibi, Profesa David Mwakyusa   (kushoto) akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Ahmed, Bungeni mjini Dodoma Juni 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BODA BODA ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUGONGANA NA LORI LA MCHANGA

 Wakiwa wanaipakiza Bodaboda hiyo baada ya ajali
 Bodaboda iliyopata ajali
 Boda Boda ikiwa inapelekwa kituo cha polisi

MAHAKAMA YAWAVUA NYADHIFA MADIWANI SITA WA BUKOBA


Hizi ni taarifa za hivi punde.Ni kutokana na sakata linaloendelea bukoba kuhusiana na mgogoro katika manispaa hiyo.
Madiwani hao kutoka vyama tofauti, walifunguliwa kesi mahakamani na Diwani wa Kata ya Kahororo, Chifu Kalumuna (CCM) kuwa hawana sifa za kuendelea kuwa madiwani.
Kalumuna, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM Manispaa ya Bukoba na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Uchumi alifungua shauri dhidi ya madiwani hao kuwa wamepoteza sifa za kuendelea kuwa madiwani kwa kushindwa kuhudhuria vikao vya kisheria bila taarifa.
Madiwani walalamikiwa katika kesi hiyo walikuwa ni Diwani Yusuph Ngaiza (Kashai CCM), Dauda Kalumuna (Ijuganyondo CCM), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo CCM) na Deusdedith Mutakyahwa wa Kata ya Nyanga CCM.
Wengine ni Richard Gaspar (Miembeni CCM), Mulungi Kichwabuta (Viti Maalumu CCM), Israel Mulaki (Kibeta CHADEMA) na Rabia Badru (Viti Maalumu CUF).
Baada ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kusoma taarifa ya ukaguzi kwenye manispaa hiyo, madiwani walitakiwa kuanza vikao mara moja.


HATIMAYE FACEBOOK WAMEVERIFY AKAUNTI YA MSANII DIAMOND,JIONEE HAPA



Hii ni neema nyingine kwa Diamond Platnumz, baada tu ya kuwa verifie kwenye mtandao wa twiter, hatimaye sasa kuwa Verified kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook,
hii inamaanisha kuwa kampuni ya Facebook hivi sasa inamtambua Diamond Platnumz kuwa kama msanii maarufu wa kimataifa, nafasi hii wanatokea kupata wasanii wachache sana na watu maarufu ambao wanapata bahati ya kujulikana na makampuni makubwa kama haya. Mwanamitindo wakimataifa Flaviana Matata ni mmoja wa watu maarufu watokao nchin Tanzania wanaotambuika na kampuni hiyo, na ni moja ya watu maarufu ambao account yao ipo Verified kama hii ya Diamond Platnumz. Huu ni mwaka mzuri sana kwa Diamond Platnumz kwa matukio yanayoendelea kumtokea, na kuzidi kumpa jina kubwa ulimwenguni kupitia muziki wake huu wa Style yake ya kipekee iliyopewa jina la AfroPop.

PICHA:::::Mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, George Mpondela yalivyokuwa








MARA BAADA YA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) KUMALIZIKA KANDA YA PWANI, WATANZANIA SASA KUANZA KUWAPIGIA KURA WASHINDI‏

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions katika Mradi wa Kusaka vipaji vya Kuigiza Nchini TMT (Tanzania Movie Talents) wakishangilia kwa kufungua Mvinyo usio na kilevi mara baada ya kumaliza zoezi la Kuzunguka Katika Kanda Sita nchini kwa kusaka Vipaji vya kuigiza ambapo zoezi hilo lilimalizika katika Kanda ya Pwani, Mkoani Dar Es Salaam ambapo washindi watano kutoka kanda ya Pwani walipatikana na Kupewa zawadi zao za Shilingi laki Tano Kila Mmoja na Kushiriki katika fainali ya Kuwania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
Mmoja wa Majaji katika Shindano la TMT Yvonne Cherry au Monalisa akifurahia kufungua Mvinyo huku wafanyakazi wa Proin wakifurahia pia kwa kukinga mvinyo huo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Pwani ambapo ndio imefunga zoezi hilo lililoanzia Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group of Companies,Bw Johnson Lukaza akiongea na wafanyakazi wa Proin Promotions limited mara baada ya kumaliza vizuri kwa kazi za kutafuta vipaji katika Kanda Sita za Tanzania.Pamoja na kuongea na wafanyakazi hao aliweza kutoa neno la shukrani kwa kila mmoja kwa kutimiza wajibu wake na hatimaye kufanikisha zoezi hilo la hatua ya kwanza kumalizika vyema.