Beki wa Manchester United, Rafael da Silva (kushoto) aliumia dhidi ya Yeovil
LOUIS van Gaal amekumbwa na majanga ya majeruhi licha ya Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi yaYeovil Town katika mechi ya raundi ya tatu ya kombe la FA.
Rafael da Silva alivujika mfupa wa taya katika kipindi cha kwanza na kutolewa wakati wa mapumziko, wakati mlinzi mwenzake Paddy McNair alihitaji bandeji kichwani kufuatia kugongana na Kieffer Moore.
Van Gaal pia alieleza kuwa beki mwingine Luke Shaw alipata majeraha
mapya ya kifundo cha mguu na yeye alitolewa wakati wa mapumziko baada ya kucheza kwa kutumia dawa ya kuzuia maumivu.
No comments:
Post a Comment