Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi, 27, amezusha tetesi
kuwa anataka kuhamia Chelsea (The Sun), Javier Hernandez- Chicharito, 26,
atauzwa na Manchester United mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake wa mkopo
utakapomalizika Real Madrid (Daily Telegraph), Tottenham na Liverpool wapo
tayari kupambana kumwania mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 21,
(Independent), Inter Milan imewapiku Liverpool kumsajili winga wa Bayern Munich
Xerdan Shaqiri, 23, (Talksport), meneja wa Juventus Massimiliano Allegri
amethibitisha kuwa klabu yake inataka kumsajili kiungo wa Galatasaray Wesley
Sneijder, 30 (Guardian), Kipa wa Arsenal Woijciech Szczesny amepigwa faini ya
pauni elfu
ishiriki kwa kuvuta sigara akiwa bafuni baada ya mechi dhidi ya
Southampton, siku ya mwaka mpya walipofungwa 2-0 (Daily Mirror), Tottenham
watawajaribu Aston Villa kwa dau la pauni milioni 3 kumtaka kiungo Fabian
Delph, 25 (Daily Mirror), Chelsea wamewazidi kete Arsenal na Liverpool katika
mbio za kumsajili kiungo wa Saint-Etienne Rayan Souici,16, ambaye amepachikwa
jia la "Paul Pogba mpya" (Daily Express), Wilfried Bony amewaambia
Swansea kuwa anataka kuhamia timu inayocheza Champions League (Daily Telegraph).
No comments:
Post a Comment