Mwalimu Gaudencia Gitano (40) anayedai kupigwa mara nyingi
na mume wake.
Akizungumza akiwa kitandani katika Hospitali ya Dar Group
iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, Gaudensia (pichani), alidai
kupigwa mara kwa mara kiasi kwamba katika vituo vya polisi na hospitali,
amekuwa ni mwenyeji.
“Mimi ni mke wa pili kati ya watatu na tulifunga ndoa
ya
kiserikali na mume wangu Colman Marwa Oktoba 25, 2002 huko Ilala Boma. Tulikuwa
tukipendana na Mungu ametujaalia tumepata watoto wawili, tulikuwa tukiishi
pamoja katika nyumba yetu huko Kitunda na baadaye tukahamia katika nyumba yetu
nyingine huko Msongola
“Kipigo kilianza mara baada ya kuoa mke wa tatu, kukawa
hakuna amani ndani ya nyumba, kila wakati ni kupigwa, nimechoka kutoa taarifa
vituo mbalimbali vya polisi na kulazwa hospitalini, nimechoka na manyanyaso,
ipo siku najua ataniua, Watanzania naombeni msaada wa kisheria kabla hajaniua.
“Huu ni mtiririko wa taarifa ya mashambulio ya kudhuru mwili
nilizokuwa nikifungua katika vituo mbalimbali vya polisi, kwa mara ya kwanza
aliponivunja mkono mwaka 2012 nilitoa taarifa katika kituo cha polisi Staki
Shari jalada Na: STK/RB/10673/2012, kipigo cha pili nilifungua jalada Na:
STK/RB/12631/2012, kilifuatia kipigo kingine nikafungua jalada No.
KIT/RB/1400/2012, katika kituo cha polisi Kitunda.
“Vipigo havikuishia hapo, mwaka 2013, nilipigwa karibia kufa
nikatoa taarifa polisi jalada Na. KIT/RB/2976/2013 na kipigo cha mwisho cha
kufungia mwaka, hadi nilipopoteza fahamu nilifungua jalada Na. STK/ RB/ 17579/
2014.
“Nakumbuka mwaka jana baada ya kuchoka na kipigo niliamua
kuondoka na kupanga Kivule, alinifuata, akanipiga na kunivunja mkono, akachukua
vitu vyangu vyote vya ndani, nilisononeka sana, nikanunua vingine, alirudi
akanipiga na kuchukua tena vitu hivyo,” alisema mwalimu huyo kwa uchungu.
Akisimulia zaidi, alisema licha ya vipigo hivyo, ambavyo
anaamini siku yoyote vitamuua, lakini mwanaume wake huyo hawajali watoto kwa
chochote, si chakula, matibabu wala mahitaji ya shuleni, ambapo kila kitu
anakifanya mwenyewe.
“Mwaka 2012 nilifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga
nikihitaji talaka, aliandikiwa barua ya wito lakini hakufika katika kesi hiyo
Na: 62, kwa hivi sasa nimechoka kwani nimekuwa nikifundisha nikiwa na manundu
sehemu mbalimbali za mwili, wanafunzi wakiniuliza nashindwa cha kuwajibu,
nawaombeni Watanzania mnisaidie kisheria, nimeshanusa kifo.
“Nitashukuru kwa watakaojitokeza kunisaidia, nawatakieni
maisha mema, nawaomba mashemeji zangu endapo Mungu atanichukua kutokana na
vipigo vya mara kwa mara, muwachukue watoto muwatunze, huyu hawezi kuwatunza.”
Mume wa mwalimu huyo, Colman Marwa alipopigiwa simu na
waandishi wetu na kuulizwa kuhusu madai hayo alijibu kijeuri. “Wewe kama
unataka kumuwekea wakili muweke, huwezi kuniuliza mimi au nenda kawe wakili
wake,CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment