Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 11, 2015

KIUNGO WA WOLFSBURG AFARIKI DUNIA

Kiungo wa klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani Junior Malanda, 20, amefariki dunia katika ajali ya gari.
Malanda, aliyekuwa akiichezea timu ya taifa ya Ubelgiji ya chini ya umri wa miaka 21, amecheza mechi 15 msimu huu katika Bundesliga na mechi za Europa League ikiwemo dhidi ya Everton.
Mkurugenzi wa michezo wa Wolfsburg Klaus Allofs amesema katika taarifa: "Tumesikitishwa sana, na hatuamini kilichotokea, hatuna hata maneno ya kusema.
"Hatuamini hayuko nasi tena. Sala zetu katika kipindi


 hiki kigumu tunazielekeza kwa familia yake."
Allofs ameongeza: "Alikuwa chachu katika timu na mwenye furaha. Junior alikuwa mchezaji kandanda mzuri sana na ambaye ndio kwanza alikuwa akichipukia."
Malanda alihusishwa na kuhamia Fulham na Crystal Palace wakati alipoondoka Zulte Waregem mwaka 2013, lakini badala yake alijiunga na Wolfsburg.
Mchezo wake wa mwisho ulikuwa dhidi ya Cologne waliposhinda 2-1 mwezi Disemba.
Polisi wa Wolfsburg wamesema Malanda alikuwa abiria katika gari lililopata ajali katika barabara kuu karibu na mji wa Bielefeld.

Alikuwa akielekea kuungana na wachezaji wenzake kabla ya kusafiri kwenda Afrika Kusini katika kambi ya mazoezi.

No comments:

Post a Comment