Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 14, 2015

MANCHESTER CITY WAKAMILISHA USAJILI WA WILFRED BONY

Manchester City wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Swansea Wilfried Bony kwa pauni milioni 28.
Bony, 26, ameingia mkataba wa miaka minne na nusu kwenda Etihad na atavaa jezi namba 14.

"Ni furaha kubwa kwangu, na heshima kubwa kuwa hapa, ni changamoto nzuri." amesema. Bony alijiunga na Swansea kwa pauni milioni 12 akitokea Vitese Arnhem mwaka 2013 na alikuwa mfungaji bora wa mwaka wa kalenda 2014 akipachika mabao 


20 katika EPL. Klabu hAzo mbili zilifikia makubaliano mwisho wa wiki, ambapo pauni milioni 25 zimelipwa taslimu, huku zilizosalia milioni 3 zitatolewa kulingana na jinsi atakavyoonesha kiwango. Uhamisho huo unafunika uhamisho wa Yaya Toure wa pauni milioni 24 mwaka 2010, na hivyo kumfanya Bony kuwa mchezaji wa gharama zaidi katika historia, kutoka Afrika.

No comments:

Post a Comment