Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 15, 2015

Msafara wa Waziri Muhongo wazomewa Kahama

Waziri wa nishati na madini Mhe. Sospeter Muhongo
WAZIRI wa nishati na madini Mhe. Sospeter Muhongo amejikuta katika wakati mgumu na msafara wake baada ya kuzomewa na wananchi wa soko la wakulima katikati ya mji wa Kahama wakati akitokea kwenye ziara yake vijijini wilayani Kahama mkoani Shinyanga
Tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na msafara wake wakitokea kata ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata ya Bulige jimbo la Msalala kukagua ujenzi wa mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na wakala wa umeme vijini nchini (REA) unaoendelea kufungwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Baada ya kufika katika eneo hilo wananchi hao 


walianza kumzomea wakidai ni “mwizi wa fedha zilikuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kelele ambazo ziliwashtua watu wengi ambao walijitokeza kuona anayezomewa ni waziri yupi.
Hata hivyo kelele hizo ziliisha baada ya msafara wa waziri huyo ambaye yuko ziara kanda ya ziwa kutokomea na kuacha makundi mbalimbali katika eneo hilo la soko la wakulima wakijadili hatima yake katika mpango mzima wa mgogolo wa uchotwaji wa mabililioni ya shilingi kwenye akaunti hiyo ya Escrow.

Pamoja na kuzomewa na wananchi hao Muhongo katika ziara yake wilayani Kahama ameacha neema kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu baada ya kuwaahidi umeme katika awamu ya tatu ya mradi ya nishati vijijini.

No comments:

Post a Comment