Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, January 15, 2015

TAZAMA PICHA JINSI WWANAFUNZI WA UDOM WALIPOFANYA MAANDAMANO JANA


 Baadhi ya wanafunzi wakiwa chini ya ulinzi wa Polisi waliokuwa wakijaribu kufanya maandamano
  Baadhi ya wanafunzi wakipanda kwenye gari la polisi baada ya kukamatwa
Baadhi ya wanafunzi waliokamatwa wakiwa kwenye gari la polisi 

Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunifu wa amani Chuoni na kufanya maandamano haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma Mjini leo tarehe 14.01.2015 majira ya 05:30hrs.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – (SACP) ameeleza kuwa chanzo cha wananfunzi hao wa programu maalum ya Diploma ya Ualimu kufanya uhalifu huo ni kikao walichofanya wananfunzi hao tarehe 13.01.201 wakidai kuongezewa posho ya chakula na kwamba hata kiasi ambacho wanapewa wamechelewa kupewa.


Hata hivyo uongozi wa Chuo uliwaeleza kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia swala la kuongezewa posho ni Bodi ya Mikopo na siyo chuo. Hivyo walitakiwa kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao. Pia walielezwa kuwa hundi kwa ajili ya fedha za posho zao zimeshasainiwa na kuwasilishwa Benki ili waweze kuanza kupewa posho zao.
Wanafunzi hao  hawakuridhika na usiku wakaanza kuhamasishana kufanya maandamano jambo ambalo ni kosa kisheria. Wanafunzi hao wamehojiwa kulingana na ushahidi ambao umekusanywa na wamefikishwa mahakamani kwa kosa la Kufanya Maandamano yasiyo na kibali. Viongozi waliohamasisha uvunjifu huo wa sheria baadi wamekamatwa na baadhi wanaendelea kutafutwa ili nao waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Ushahidi uliokusanywa unaonyesha jinsi viongozi hao wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao rasmi na visivyo rasmi, katika vikundi, kupita katika mabweni na kutuma sms.
Kamanda MISIME ametoa wito kwa Wanafunzi hao kutumia taratibu zilizowekwa na Serikali na Chuo kuwasilisha malalamiko yao ngazi kwa ngazi na siyo kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo vitawasababishia kukamatwa. Endapo watafanya hivyo wasije kulaumu mtu kwani hatua zitachukuliwa kulingana na Sheria inavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment