Mtoto Emmanuel Mwingira (7) mkazi wa mtaa wa Kiwandani Mbinga mjini,
akiwa amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Mbinga mkoa wa Ruvuma,
baada ya kulipukiwa na Vilipushi[detonator] ambavyo vimesadikiwa kuwa
hutumika kulipulia miamba, wakati alipokuwa akicheza nawenzake na
kusababisha kuumia mkono wake wa kulia na sehemu mbalimbali zamwili
wake. Huyo ni mmoja kati ya watoto sita ambao walio patwa na mkasa huo
.Picha NA AMON MTEGA
NA AMON MTEGA wa Demashonews
WATOTO wanne kati ya sita wamenusurika kifo, wilaya Mbinga mkoani
Ruvuma baada ya kuwalipukia viripushi vinavyodaiwa kuwa ni vya
kulipulia miamba ( detonator) ambavyo vimewajeruhi vibaya, wakati
mwenzao mmoja akiwa amekishika na kunganisha nyaya na betri na nyaya
walipokuwa wanacheza pamoja.
Akiongea na wandishi wa habari jana ofisini kwake kamanda wa Polisi
wa mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela, alisema kuwa, tukio hilo lilitokea
Kiwandani mjini Mbinga, wakati watoto hao wakiwa wanachezea vilipushi
hivyo walivyoviokota kwenye jalala.
Msikhela alikitaja kitu hicho kuwa ni vilipushi ambavyo vinadaiwa kuwa
vinatumika na watafiti wa madini migodini au walipuaji baruti, huku
akieleza kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya ambapo liliwakumba watoto
Alisema kuwa vilipushi hivyo hivyo havihusiani kabisa na masuala ya
mabomu kama baadhi ya watu walikuwa wakidhania kuwa ni bomu kumbe
sivyo
Akiwataja watoto waliolipuliwa kuwa ni Philiberth Mbungu (10),
Augustino Millanzi (5), Geofrey Ndunguru (8) na Emmanuel Mwingira (7)
ambao wote wameumizwa sehemu mbalimbali huku wengine wawili Ayubu
Methew (10) na Hassan Mapangi (5) wakiwa na majeraha ya kawaida
mwilini.
Msikhela alifafanua kuwa mfawidhi wa mtoto Philiberth na Augustino
wamepelekwa katika hospitali ya mkoa Songea kwa matibabu zaidi kwa
kuwa walikuwa wamejeruhiwa vibaya sehemu za usoni ,machoni .
Aidha alisema kuwa Geofrey na Emmanuel wanaendelea kupatiwa matibabu
katika hospitali ya wilaya ya Mbinga, ambapo nao wamejeruhiwa usoni na
mikononi na wanaendelea na matibabu.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alisema uchunguzi
unaendelea juu ya tukio hilo na alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo
kuwa waangalifu na watoto wasiwaachie wakitembea hovyo, hivyo pale
wanapoona kitu chenye muunganiko wa nyaya wasikiguse bali watoe
taarifa mapema kwenye vyombo vya usalama ambavyo vipo karibu nao.
No comments:
Post a Comment