Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau.kundi hilo
limedaiwa kuwateka vijana 40 katika kijiji cha Malari kazkazini mwa Nigeria
Takriban wavulana 40 na vijana wadogo wameripotiwa kutekwa
nyara na wapiganaji wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Wakaazi waliokitoroka kijiji cha Malari na kuwasili katika
mji wa Maiduguri siku ya ijumaa usiku wanasema kuwa kitendo hicho kilitekelezwa
siku moja tu kabla ya mwaka mpya.
Wanasema kuwa watu waliojihami waliwasili katika kijiji
hicho katika gari aina ya pick up na kuwaagiza
wanaume wote kutoka nje ili
kuweza kusikiliza mahubiri.
Vijana wadogo baadaye walizungukwa na kupelekwa katika msitu
jirani wa Sambisa.
Mwaka uliopita kundi hilo la Boko haram liliwateka nyara
zaidi ya wasichana 200 kutoka shule moja ya bweni kazkazini mwa Nigeria.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment