Singapore inaadhimisha miaka hamsini ya taifa hilo mwaka
2015, na serikali ya nchini hiyo inapanga kutoa zawadi maalum kwa kila mtoto
atakayezaliwa mwaka huu kuadhimisha ngwe hiyo.
Watoto watakaozaliwa mwaka huu 'watakaribishwa' duniani kwa
kupewa kiboksi cha zawadi chenye mahitaji muhimu ambayo wananchi wamependekeza.
Kwa mujibu wa tovuti inayoshughulikia mradi huo, zawadi hizo ni pamoja na
kumbwewe ya kubebea mtoto, mfuko wa kuwekea nguo za mtoto, na nguo zenye
maandishi yasemayo "Mimi ni mtoto wa jubilei ya dhahabu". Wazazi pia
watapatiwa kitabu cha
kuandika matukio muhimu ya kukumbuka, na pia tuzo maalum
ya ukumbusho.
Vitu hivyo vilipendekezwa na wananchi mbalimbali, na vina
lengo la kuashiria "kila mema kutoka kizazi hiki kwenda kijacho"
imekaririwa tovuti hiyo.
Mradi huu ni kwa watoto wote raia wa Singapore watakaozaliwa
kuanzia Januari 1 2015, ikiwa ni pamoja na hata wanaozaliwa nje ya nchi lakini
ni raia wa Singapore, serikali imesema. Na zawadi huenda zikaongezeka kwa
watoto wa mwaka huu nchini humo kwani zawadi zaidi zimeahidiwa na benki kadhaa.
No comments:
Post a Comment