Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 16, 2015

BAADA YA MCHINA HUYU KUSHINDWA KUMILIKI LAMBORGHINI AKAANUA KUFANYA HIVI,JIONEE HAPA

Baada ya kuwa na ndoto za kuendesha gari ya kifahari aina ya Lamborghin huku akiwa hana uwezo wa kununua gari hiyo Yu Jietao raia wa Jiangx, China amewashangaza watu wengi baada ya kuja na staili yake ya kutengeneze gari kama hiyo ili atimize ndoto zake.
Jamaa huyo alifikia uamuazi wa kutumia mbao na kutengeneza gari yenye muundo wa Lamborghin 



baada ya kuona hana uwezo wa kumudu gharama za gari hilo zinzofikia Euro 260,000 hivyo akaamua kufanya hivyo ili kulinganisha na gari hiyo yenye thamani.
Kwa kutumia taaluma yake ya ufundi seremala Jietao aliamua kutafuta mbao na kutengeneza gari lenye kufanana kabisa na gari hiyo huku akiweka vifaa vingine vyote vinavyowezesha gari hiyo kutembea na kufanya kazi kama kawaida.

Muenekano wa gari hiyo umekua kivutio kikubwa kwa watu wengi huku wakijaribu kutaka kulinunua kwa gharama kubwa lakini mwenyewe amesema hawezi kuliuza.

No comments:

Post a Comment