Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 16, 2015

Mtoto wa Jackie Chan aongea na waandishi wa habari baada ya kutoka jela..

Habari ya  kuachiliwa kwa mtoto wa actor Jackie Chan ambaye alikamatwa kwa kosa la kukutwa na bangi nyumbani kwake na pia kosa la kuruhusu watu wavute bangi nyumbani kwake.
 Jaycee Chan ameongea na waandishi wa Habari na kuomba radhi kwa kosa hilo ambalo limemfanya akae jela kwa miezi sita.
 Kama mtu ambaye ni staa kwenye jamii yake anaamini kwamba makosa yake yamemfanya aonekane mtu tofauti kwenye jamii yake.


Jackie Chan ni Balozi wa mapambano ya dawa za kulevya China tangu mwaka 2009, lakini hakuwahi kufanya ushawishi wowote ili mtoto wake aachiwe gerezani.


Watu wa China wanahisi Chan kaachiwa mapema kwa sababu baba yake ni mtu mwenye ukaribu mkubwa na viongozi wa juu wa Serikali ya nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment