Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, February 7, 2015

Benki ya Marekani yafunga huduma zake nchini Somalia

Huduma za benki nchini Somalia
Serikali ya Somalia imesema kuwa uamuzi wa benki moja nchini Marekani kufunga akaunti za kampuni za kuhamisha fedha nchini Somalia utaathiri usalama ulioafikiwa nchini humo.
Benki ya Merchants kutoka jimbo la Carlifornia,ambayo husimamia asilimia 80 ya fedha zote zinazoelekea nchini Somalia, imesema kuwa


 inaondoa huduma zake nchini humo kutokana na madai ya mapya ya biashara ya fedha chafu.
Mwakilishi wa umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay ,amesema kuwa hatua hiyo inaleta wasiwasi mkubwa kwa kuwa usafirishaji huo wa fedha ndio mfumo wa maisha ya raia wa Somalia.

Raia wa Somalia nchini Marekani hutuma nyumbani zaidi ya dola millioni 200 kila mwaka.

No comments:

Post a Comment